Waberberi

Context of Waberberi

Waberberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Moroko hadi Misri na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru".

Kabila lao mojawapo linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.

Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wamezoea kutumia lugha ya Kiarabu, hivyo wanahesabiwa kati ya Waarabu.

Wanaoendelea kutumia lugha ya Tamazight (au: Kiberber) kama lugha ya kwanza ni:

 • takriban theluthi ya watu huko Moroko,
 • asilimia 10-15 nchini Algeria,
 • labda asilimia 3 nchini Libya,
 • idadi ndogo zaidi wako Tunisia,
 • laki kadhaa huishi katika nchi za Sahara kama Mali na Niger halafu
 • wako kwa idadi ndogo Burkina Faso, Misri na Mauritania.
 • Kutokana na uhamiaji kuna nusu milioni nchini Ufaransa.

Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani wanalima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoe...Read more

Waberberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Moroko hadi Misri na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru".

Kabila lao mojawapo linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.

Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wamezoea kutumia lugha ya Kiarabu, hivyo wanahesabiwa kati ya Waarabu.

Wanaoendelea kutumia lugha ya Tamazight (au: Kiberber) kama lugha ya kwanza ni:

 • takriban theluthi ya watu huko Moroko,
 • asilimia 10-15 nchini Algeria,
 • labda asilimia 3 nchini Libya,
 • idadi ndogo zaidi wako Tunisia,
 • laki kadhaa huishi katika nchi za Sahara kama Mali na Niger halafu
 • wako kwa idadi ndogo Burkina Faso, Misri na Mauritania.
 • Kutokana na uhamiaji kuna nusu milioni nchini Ufaransa.

Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani wanalima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoendelea na maisha ya kuhamahama.

More about Waberberi

Map