Jamhuri ya Watu wa China

Context of Jamhuri ya Watu wa China

China (pia: Uchina, Sina; kirefu: Jamhuri ya Watu wa China) ni nchi kubwa ya Asia ya Mashariki ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote duniani.

China imepakana na Vietnam, Laos, Myanmar, India, Bhutan, Nepal, Pakistan, Afghanistan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Kazakhstan, Urusi, Mongolia, Korea ya Kaskazini.

Kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China ambazo ni bahari ya kando ya Pasifiki.

China kuna makabila 56 tofauti. Wahan ndio kabila kubwa zaidi nchini China kwa idadi ya watu ikiwa na asilimia 92.

Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin kinachotumiwa na asilimia 70 za wananchi.

Siasa inatawaliwa na chama cha kikomunisti.

Mji mkuu ni Beijing lakini Shanghai ndio mji mkubwa zaidi.

Hong Kong iliyokuwa koloni la Uingereza na Macau iliyokuwa koloni la Ureno ni maeneo ya China yenye utawala wa pekee.

Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazam...Read more

Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazamwa na serikali ya Beijing kuwa majimbo yake lakini vimekuwa kama nchi ya pekee tangu mwaka 1949.

More about Jamhuri ya Watu wa China

Map

Videos