Kikatalunya

Kikatalunya

Kikatalunya au kikatalani ("català") ni mojawapo kati ya lugha za Kirumi ambayo ni lugha rasmi ya jimbo la Katalunya, Valencia na visiwa wa Baleari katika ufalme wa Hispania (Ulaya kusini magharibi) na vilevile utemi wa Andorra. Pia inatumika katika sehemu za Ufaransa kusini na Italia visiwani.

Wanaoitumia kama lugha ya kwanza ni watu milioni 4.1 na kama lugha ya pili ni milioni 5.1.